Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda siku ya Jumamosi waliuteka mji wa kimkakati huko Goma Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo// Huko Kenya vijana wanne waliodaiwa kutoweka Disemba mwaka jana wamepatikana huku wengine watatu bado hawajulikani waliko// Pazia la uchaguzi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema kwa wagombea wake kuchukua na kurejesha fomu limefungwa.