Rais mteule wa Marekani Donald Trump ataka viongozi wa upinzani Venezuela walindwe huku rais Nicholas Maduro akiapishwa leo. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron azungumza na waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer kuhusu Ukraine na Mashariki ya Kati. Na China yaahidi kulisaidia bara la Afrika na msaada wa kijeshi.