Kumekuwa na miito kutoka pande tofauti za ulimwengu za kuitaka serikali ya Tanzania kukamilisha mchakato wa kukabidhiana madaraka kwa amani, baada ya kifo cha rais wa taifa hilo John Pombe Magufuli kilichokea baada ya kutoonekana hadharani kwa takribani siku 18, na kuzusha hofu ya hali ya afya yake.