Waarmenia duniani kote wamefanya kumbukumbu ya miaka 100 tangu kuanza kwa mauaji yaliyofanywa na utawala wa himaya ya Ottoman wa Uturuki ya Karibu watu milioni 1.5. Katika mjadala bungeni jana (24.04.2015)mjini Berlin, spika wa bunge la Ujerumani Bundestag Norbert Lammert ameyaeleza mauaji hayo kuwa ni mauaji ya kimbari.