1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tchiani apanga kuunda serikali ya mpito kwa miaka 3 Niger

20 Agosti 2023

Kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Niger Abdourahamane Tchiani anataka kuunda serikali ya mpito itakayokuwa madarakani sio zaidi ya miaka mitatu.

https://p.dw.com/p/4VN8Y
Niger | General Tchiani übernimmt Macht nach Putsch gegen Präsident Bazoum
Picha: ORTN/Télé Sahel/AFP/Getty Images

Akizungumza kupitia televisheni ya taifa Tchiani ameonya pia kuhusu mataifa ya nje kuingilia masuala ya ndani ya taifa hilo.  

Kabla ya mpango wake huo, Tchiani amesema ataandaa mazungumzo ya kitaifa ndani ya siku 30 kulijadili hilo na Wa-Niger wote. Mazungumzo hayo yatatoa muelekeo wa kuundwa kwa katiba mpya.  

Kiongozi wa mapinduzi Niger kuunda serikali ya mpito

Tangazo lake limejiri baada ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kusema kuwa viongozi wake wa ulinzi wanapanga kuuingilia mzozo huo iwapo uongozi unaozingatia katiba hautarejeshwa nchini humo. 

Jenerali Tchiani aliingia madarakani mwezi uliopita baada ya mapinduziwakati walinzi wa rais walipomkamata rais Mohammed Bazoum na kuchukua madaraka.