1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA : Ajali ya ndege yauwa 99 Nigeria

30 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxq

Ndege ya abiria nchini Nigeria imeanguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka katika mji mkuu wa Abuja hapo jana na kuuwa watu 99 akiwemo kiongozi wa Waislamu milioni 70 nchini humo.

Maafisa wanasema kulikuwa na abiria 106 kwenye ndege hiyo aina ya Boeing 737 katika safari ya kuelekea katika mji wa kaskazini wa Sokoto wakati ilipoanguka kwenye shamba ka nafaka kama kilomita 2 kutoka njia ya kurukia na kutulia ndege.Watu saba walinusurika katika ajali hiyo.

Miongoni mwa watu waliokufa ni Ibrahim Muhammadu ambaye akiwa Sultani wa Sokoto alikuwa kiongozi wa jamii ya Waislamu wa Nigeria ambao idadi yao ni nusu ya wananchi wa taifa hilo lenye idadi kubwa kabisa ya watu barani Afrika.

Vitu pekee viliyopweza kujulikana kwenye eneo la ajali ni mkia wa ndege hiyo,engine na sehemu ya bawa la ndege.

Hii ni ajali ya nne ya ndege nchini Nigeria katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo watu 335 wamepoteza maisha yao.