ABUJA: Daktari wa Kimarekani azuiliwa Nigeria
9 Agosti 2005Matangazo
Maafisa wa forodha nchini Nigeria wamesema daktari mmoja wa Kimarekani amezuiliwa kwa sababu ya kuingiza nchini humo risasi za bunduki kwa njia isiyo halali.Daktari huyo anaeajiriwa na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Jos nchini Nigeria alizuiliwa kwenye ofisi ya posta alipokwenda kuchukua mzigo uliokuwa na risasi.Maafisa wa forodha wamesema mzigo huo ulielezwa kuwa na vyombo vya ufinyanzi na chokoleti.Msemaji wa ubalozi wa Marekani nchini Nigeria amethibitisha kuwa daktari huyo alikamatwa tarehe mosi Agosti na yungali kizuizini.