ABUJA: Kituo cha mafuta kimevamiwa kusini mwa Nigeria
12 Novemba 2006Matangazo
Watu wenye silaha wamekivamia kituo cha kutoa mafuta kwenye Niger Delta,kusini mwa Nigeria na wamewateka nyara wafanyakazi kadhaa.Kwa mujibu wa duru za sekta ya mafuta,shambulio hilo katika kituo cha mafuta kwenye jimbo la Bayelsa limetokea wakati ambapo kituo kingine cha mafuta katika jimbo hilo kimekaliwa na waandamanaji wanaotaka kulipiwa fidia kwa uchafuzi wa mafuta uliofanywa sehemu hizo.Msemaji wa serikali ya jimbo la Bayelsa amethibitisha kuwa shambulio hilo lilitokea siku ya jumamosi lakini hakuwa na maelezo zaidi.Kituo hicho cha mafuta sasa kimeshambuliwa kwa mara ya pili katika muda wa majuma mawili.Matatizo hayo yanasababishwa na mgogoro wa muda mrefu kati ya kampuni ya mafuta na wakazi wa vijijini.