ABUJA: Mahabusu wa kigeni 12 wameachiliwa huru Nigeria
12 Juni 2007Matangazo
Wanamgambo katika Niger Delta,eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta nchini Nigeria,wamewaachilia huru mahabusu 12 wa kigeni na Mnigeria mmoja.Kwa mujibu wa maafisa,kundi hilo la Wamarekani 3, Waingereza 5,Wahindi 2,Mfilipino na raia mmoja wa Afrika ya Kusini,liliachiliwa huru Jumatatu usiku katika jimbo la Bayelsa kusini mwa nchi. Wafanyakazi hao wa kigeni walikamatwa majuma ya hivi karibuni,katika mashambulizi mbali mbali ya uvamizi.Bado kama wafanyakazi 20 wa kigeni wamezuiliwa katika eneo hilo.Katika kipindi cha miezi 18 iliyopita,zaidi ya wageni 200,wengi wao wakiwa wafanyakazi wa makampuni ya mafuta ya kigeni,wametekwa nyara nchini Nigeria.