ABUJA: Mahabusu wa kigeni waachiliwa huru Nigeria
22 Oktoba 2006Matangazo
Wanamgambo kusini mwa Nigeria wamewaachilia huru wafanyakazi 7 wa kigeni wa kampuni ya mafuta. ExxonMobil imesema imearifiwa na maafisa wa Nigeria kuwa wafanyakazi wote 7 wapo katika hali nzuri ya afya.Mateka hao waliachiliwa huru mji wa Eket,walikotekwa nyara majuma mawili ya nyuma na sasa wanarejea makwao.Wanne ni kutoka Scotland, na wengine watatu ni kutoka Indonesia,Rumania na Malaysia.Uzalishaji wa mafuta nchini Nigeria umepunguka kwa takriban robo moja kwa sababu ya mashambulio ya hivi karibuni ya makundi ya wanamgambo.