1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA: Mwanamke afa kwa homa ya ndege nchini Nigeria.

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVA

Uchunguzi umethibitisha msichana mwenye umri wa miaka ishirini na miwili aliyefariki nchini Nigeria majuma mawili yaliyopita, alikuwa na virusi vya homa ya ndege.

Shirika la afya duniani, WHO, limetoa taarifa kwenye mtandao likisema watu wote waliokuwa wakiishi pamoja na msichana huyo kabla ya kifo chake, hawajapatikana na virusi hivyo.

Taarifa hiyo pia imesema uchunguzi unafanywa kutambua asili ya maambukizi hayo.