ABUJA: Nigeria yaomboleza rasmi vifo vya watu 117
25 Oktoba 2005Matangazo
Nigeria imetangaza siku tatu za kuomboleza vifo vya watu 117 vilivyotokea katika ajali ya ndege siku ya Jumamosi.Ndege aina ya Boeing 737 ya shirika la Bellview Airlines ilikuwa njiani kwenda mji mkuu wa Nigeria Abuja,ilipoanguka nje ya mji wa Lagos.Sababu ya ajali hiyo ingali ikichunguzwa.Ripoti za hapo awali zilisema kuwa walikuwepo watu walionusurika,lakini maafisa waliokuwepo kule ndege ilikoangukia wamesema, hakuna ye yote alienusurika katika ajali hiyo.Kwa mujibu wa baadhi ya vyombo vya habari,maafisa wakuu wa Nigeria na wajumbe wa ngazi ya juu wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi-ECOWAS ni miongoni mwa abiria waliofariki.