1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA: Rushwa nchini Nigeria

6 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFPv

Spika wa bunge la Nigeria Adolphus Wabara amejiuzulu wadhifa wake kufuatia madai ya kuhusika na ulaji rushwa.

Wabara ameshutumiwa kuchukua zaidi ya Euro laki tatu kupitisha mswaada wa bajeti ya elimu.

Wabara amesema amejiuzu ili aweze kujitetea na madai hayo.

Katika juhudi za kumaliza rushwa nchini humo rais Olusegun Obasanjo amemfuta kazi waziri wake wa ujenzi wa nyumba juu ya jaribio la kuuzakwa siri bidhaa kwa maafisa wakuu nchini humo.

Wakati huo huo aliyekuwa mkuu wa polisi pia ameshtakiwa kwa kufuja Euro milioni 78.

Shirika la Transparency Internationl la Berlin limeitaja Nigeria kuwa nchi ya tatu duniani inayoongoza katika rushwa.