1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abuja. Umoja wa Afrika warefusha muda wa majeshi yake Darfur.

1 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnk

Ripoti kutoka mjini Abuja zinasema kuwa umoja wa Afrika umerefusha kwa muda wa miezi sita muda wa jeshi la kulinda amani la umoja huo katika jimbo la Darfur, jimbo ambalo limekumbwa na vita magharibi ya Sudan.

Msemaji wa umoja wa Afrika amesema kuwa hakukuwa na makubaliano ya kuongeza ukubwa wa jeshi hilo kupindukia wanajeshi 7,000.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir ameondoka mjini Abuja kwa mara nyingine tena akikataa kuongezwa kwa majeshi ya umoja wa mataifa.

Bashir amesema umoja wa mataifa unapaswa tu kutuma msaada wa kiufundi na fedha. Mzozo wa Darfur baina ya serikali na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali dhidi ya waasi umesababisha watu milioni 2.5 kuhama makaazi yao na watu wengine 200,000 wameuwawa.

Mjini Geneva mataifa 29 wanachama wa baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa wametaka kufanyike kikao cha dharura kuhusu Darfur.

Finnland inasema kuwa hali ni mbaya sana katika jimbo hilo.