ABUJA: Wafanyakazi wa kigeni watekwanyara Nigeria
2 Novemba 2006Matangazo
Muingereza mmoja na Mmarekani wametekwa nyara kutoka meli yao nje ya pwani ya jimbo la Bayelsa kusini mwa Nigeria.Kwa sababu ya wimbi la utekejai nyara na mashambulio yanayoendelea kufanywa dhidi ya wageni katika eneo la Niger Delta,mamia ya wafanyakazi wa kigeni wamelazimika kuondoka kutoka eneo hilo lililokuwa na utajiri wa mafuta.Vile vile uzalishaji wa mafuta ya Nigeria umepunguka kwa mapipa 500,000 kwa kila siku moja.