1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA Wajerumani wawili watekwa nyara nchini Nigeria

16 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF37

Kundi la wanamgambo katika eneo lenye mafuta mengi la Niger Delta nchini Nigeria, limewateka nyara wajerumani wawili na wanigeria wanne wanaolifanyia kazi kampuni la ujenzi linalotoa huduma kwa kampuni kubwa la mafuta la Shell.

Afisa wa kampuni hilo amethibitisha kwamba wafanyakazi hao sita wa kampuni la Ujerumani la B&B, walitekwa nyara wakati walipokuwa wakisafiri kwa dau kusini mwa nchi hiyo.

Mizozo kati ya makampuni ya mafuta ya kigeni na wanamgambo hutokea mara kwa mara katika eneo hilo la Niger Delta, ambalo hutoa karibu mapipa yote milioni 2.3 ya mafuta ya mataifa wanachama wa jumuiya ya nchi zinazosafirisha mafuta duniani, OPEC.