ABUJA: Yar'Adua ameapishwa Rais mpya wa Nigeria
29 Mei 2007Matangazo
Umaru Yar’Adua ameapishwa kama rais mpya wa Nigeria.Katika sherehe iliyofanywa mji mkuu Abuja Yar’Adua alipokea wadhifa wa urais akimrithi Olusegun Obasanjo alieondoka madarakani.Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Nigeria kwa viongozi wa kiraia kupokezana madaraka.Yar’Adua ameahidi kuendelea na mageuzi ya kiuchumi yalioanzishwa na Obasanjo.Makundi ya upinzani yameshutumu kuwa uchaguzi wa mwezi uliopita ulifanyiwa udanganyifu.Wasimamizi wa kimataifa wamesema,uchaguzi huo si wa kuaminika.