1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abuja - Yar'adua atangazwa Rais Nigeria

23 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7n

Tume ya uchaguzi nchini Nigeria imemtangaza Bwana Umar Musa Yaradua kuwa mshindi katika uchaguzi wa Urais wa nchi hiyo uliofanyika jumamosi iliyopita.

Kwa mujibu wa tume hiyo, Bwana Yaradua wa chama tawala cha PDP amepata zaidi ya kura milioni 24 akifuatiwa na Muhamad Buhari wa chama cha ANPP, aliyepata kura milioni 6.

Wawakilishi kutoka umoja wa nchi za ulaya pamoja na wale wa jumuiya ya madola , wamesema uchaguzi huo uliandamwa na mizengwe , kuambatana na vurugu, na ukosefu wa vifaa vya kupigia kura katika baadhi ya vituo.