ABUJA:40 wameshakufa kutokana na ghasia zinazoandamana na uchaguzi nchini Nigeria
16 Aprili 2007Matangazo
Watu zaidi ya 40 wamekufa kutokana na ghasia zilizoandamana na uchaguzi wa wabunge na magavana nchini Nigeria.
Matokeo ya awali yameonesha kuwa chama kinachotawala cha PDP kinaongoza katika majimbo sita kati ya manane ambapo kura zimehesabiwa .
Habari juu ya matokeo hayo zimesababisha ghasia katika mitaa kadhaa.Wapinzani wa serikali walichoma moto majengo na kuweka vizuizi barabarani.
Hatahivyo rais Olusegun Obasanjo amesema anatumai kuwa matokeo ya uchaguzi huo yatakuwa halali.