ABUJA:Atiku Abubakar aruhusiwa kogembea ,Nigeria
18 Aprili 2007Matangazo
Tume ya uchaguzi nchini Nigeria imemruhusu makamu wa rais wa nchi hiyo bwana Atiku Abubakar kugombea katika uchaguzi wa rais wakati zimebakia siki tatu tu.
Tume hiyo imelazimika kumruhusu bwana Abubakar kogembea baada ya mahakama kuu ya Nigeria kutoa uamuzi huo.Hapo awali tume hiyo ya uchaguzi iliondoa jina la bwana Abubakar kwenye orodha ya wagombea.
Mahakama kuu imesema kuwa tume hiyo haina mamlaka ya kumnyima makamu wa rais huyo haki ya kusimama katika uchaguzi.