Abuja.Helikopta yaanguka na kuua mtu mmoja nchini Nigeria.
10 Novemba 2006Matangazo
Mtu mmoja amefariki na wengine watatu wamejeruhiwa vibaya, wakati helikopta iliyokodiwa ilipoanguka karibu na kusini- magharibi mwa Nigeria katika mji wenye mafuta wa Wari.
Kuanguka kwa helikopta hiyo inayofanyakazi maeneo ya jangwani kumetokea siku 12 baada ya kuanguka kwa ndege ya abiria iliyouwa watu 96 karibu na mji mkuu wa Nigeria, Abuja mara tu baada ya kuruka.
Mwili wa mtu aliyefariki hadi hivi sasa bado haujafahamika.