1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA:Malkia Elizabeth aipongeza Nigeria

4 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFvS

Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza hapo jana amepongeza kurudi kwa utawala wa kuchaguliwa nchini Nigeria akiwa katika ziara yake ya kwanza ya nchi hiyo yenye idadi kubwa kabisa ya watu barani Afrika tokea ilipojipatia uhuru wake kutoka Uingereza zaidi ya miongo minne iliopita. Taifa hilo kubwa la Afrika Magharibi limepitia historia ya machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe,mapinduzi ya kijeshi na rushwa tokea ilipopata uhuru wake na wengi wanaiwekea matumaini kwa kipindi chake cha miaka mitano cha majaribio cha hivi karibuni katika demokrasia. Ameuambia umati wa wageni waalikwa 1,500 katika dhifa ya kitaifa kwenye viwanja vya nyumba ya Rais Olesegun Obasanjo kwamba Uingereza na sehemu kubwa ya jumuiya ya kimataifa imefurahia kurudi kwa Nigeria katika utawala wa kidemokrasia hapo mwaka 1999 na kwamba wanakaribisha mipango ya serikali ya nchi hiyo kwa mageuzi yanayohitajika mno ya kisiasa,kiuchumi na mahkama. Malkia Elizabeth amechaguwa tukio la Mkutano wa Viongozi wa Serikali wa Jumuiya ya Madola ambao ataufunguwa hapo kesho kufanya ziara yake ya kwanza nchini Nigeria tokea mwaka 1956 miaka minne baada ya nchi hiyo kujipatia uhuru wake.