ABUJA:Mgomo Nigeria
20 Juni 2007Matangazo
Mgomo wa Wafanyikazi umeanza nchini Nigeria.
Mgomo huo ambao haujulikani utamalizika lini huenda ukalemaza shughuli nyingi katika taifa hilo la Africa linalotoa kiasi kikubwa cha mafuta.
Vyama vya wafanyikazi vimekataa mapendekezo ya serikali ya kutaka kufikiwa makubaliano vikisema ni hatua iliyokuja kuchelewa.
Vyama hivyo vimewataka wafanyikazi wa Benki,shule na masoko nchini humo kushiriki mgomo huo.
Wafanyikazi wanapinga kima cha chini cha mishahara, kiasi kikubwa cha kodi ,kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli pamoja na ubinafisishaji wa kampuni mbili za mafuta.
Serikali hapo jana ilisema itaongeza mshahara kwa asilimia 15 na kupunguza kodi ya ongezeko la thamani kutoka asilimia 10 hadi asilimia tano.