1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJAMtoto wa kike aliyekuwa katekwa nyara Nigeria aachiwa huru

9 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkd

Waasi nchini Nigeria hatimaye wamemuachia huru msichana mdogo wa kiingereza waliyekuwa wamemteka nyara kusini mwa mji wa Port Harcourt alhamisi iliyopita.

Kwa mujibu wa msemaji wa eneo hilo mtoto Margaret Hill mwenye umri wa miaka mitatu yuko kwenye hali nzuri ya kiafya na ameshaunganishwa na familia yake. Watekaji nyara walitishia kumuua ikiwa hawatopewa malipo ya kumuachilia au babake mtoto huyo kuchukua mahala pa mwanawe.

Utekaji nyara wa aina hiyo umeenea kwenye eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Niger Delta ,lakini utekaji nyara wa mtoto huyo umewakasirisha makundi ya wapiganaji kwenye eneo hilo ambao wanasema unahujumu juhudi zao za kudhibiti kikamilifu mapato ya mafuta katika sehemu hiyo.