Abuja.Rais wa Nigeria atka kufanyika uchunguzi wa ajali ya ndege iliyouwa watu 100.
30 Oktoba 2006Matangazo
Rais Olusagun Obasanjo wa Nigeria ameamuru uchunguzi kamili ufanywe na kutangaza siku tano za msiba baada ya ajali ya ndege iliyotokea jana katika mji mkuu huo.
Watu mia moja wanahofiwa wamekufa ikiwa ni pamoja na kiongozi wa kiislamu mfalme wa Sokoto nchini humo na wanasiasa kadhaa wa kaskazini na watu sita wamesalimika.
Ndege hiyo chapa Boing 737 ya shirika la ADC imeanguka muda mfupi baada ya kuruka toka Abuja ikiwa njiani kuelekea Sokoto.