ABUJA:Waangalizi wa EU wawasili Nigeria
28 Machi 2007Ujumbe wa Umoja wa Ulaya unaosimamia uchaguzi nchini Nigeria unapeleka waangalizi nchini humo huku uchaguzi wa wabunge ukisubiriwa kufanyika mwezi ujao.Kulingana na ujumbe huo waangalizi 66 wanajiandaa kwa shughuli hiyo kote nchini humo.
Kwa mujibu wa mwangalizi mkuu Max van den Berg kundi lake halitatekeleza shughuli hiyo katika eneo la mafuta mengi la Niger Delta ambako wafanyikazi wa kigeni katika viwanda vya mafuta hukamatwamara kwa mara.
Ujumbe huo unatarajiwa kutoa taarifa ya uchaguzi kila baada ya sehemu ya uchaguzi kufanyika katika kipindi cha mezi mitatu ya shughuli hiyo vilevile itakapokamilika.
Uchaguzi wa wabunge unafanyika mwezi ujao tarehe 14 huku uchaguzi wa rais kufanyika mwezi huohuo tarehe 21.Hii ni mara ya kwanza nchi ya Nigeria inamaliza utawala usio wa kijeshi na kuingia utawala usio wa kijeshi tangu kupata uhuru mwaka 1960.