ABUJA:Wafanyakazi 60 wa kampuni ya mafuta watekwa nyara nchini Nigeria
11 Oktoba 2006Matangazo
Watu sitini wanaofanya kazi katika sekta ya mafuta wametekwa nyara katika jimbo la Delta, nchini Nigeria. Msemaji wa kampuni ya mafuta ya Shell ameeleza kuwa watu hao ni wafanyakazi wa tawi la kampuni hiyo ya Shell katika jimbo hilo .
Watu hao wameshikiliwa kwenye kituo kimoja cha mafuta na kwamba bado wapo katika hali nzuri ya afya.
Matukio ya utekaji nyara yamekuwa yanafanywa mara kwa mara na watu wanaopigania haki ya kuwa na usemi katika utajiri wa mafuta kwenye jimbo hilo la Delta nchini Nigeria.