1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACCRA: Mutano wa kilele wa Umoja wa Afrika waingia siku ya pili

2 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmh

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika umeingia siku yake ya pili hii leo mjini Accra Ghana.

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema bara la Afrika linahitaji kuungana pamoja huku akionya kwamba hakuna kiwango chochote cha msaada kutoka nje kitakacholikwamua bara hilo kutokana na matatizo yanayolikabili.

Mkutano huo wa siku tatu mjini Accra unaangaliwa kama nafasi ya kuunda muungano wa nchi za Afrika, huku rais wa Libya, Muamar Ghadafi, akitaka kuwepo na sera moja ya kigeni na ulinzi.

Akiufungua mkutano wa Accra, mwenyekiti wa halmashauri ya Umoja wa Afrika, Alpha Oumar Konare, alilaani shambulio la roketi dhidi ya ndege ya waziri mkuu wa Ivory Coast, Guillaume Soro, lililofanywa Ijumaa wiki iliyopita, ambapo wapambe wanne waliuwawa.

Konare alisema shambulio hilo linadhihirisha haja ya kuharakisha mchakato wa kutafuta amani na kuwapokonya silaha waasi nchini Ivory Coast, kulingana na mkataba uliosainiwa mwezi Machi mwaka huu unaolenga kuliunganisha eneo linalodhibitiwa na waasi na eneo la serikali.