1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika lakutana

13 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJc

Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika linakutana leo mjini Addis Ababa, Ethiopia kuzungumzia mzozo wa Darfur.

Mkutano huo unafanyika baada ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuishutumu serikali ya Sudan kwa kuchochea na kushiriki katika vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur.

Ripoti iliyowasilishwa kwenye mkutano uliofanyika jana mjini Geneva Uswissi, ilisema hatua zilizochukuliwa na jumuiya ya kimatiafa zimeshindwa kuzuia ubakaji, mateso na vitendo vingine viovu dhidi ya raia wa Darfur.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema yuko tayari kwenda Khartoum kuzungumzo na viongozi wa Sudan.

Kwa mujibu wa makadirio ya Umoja wa Mataifa, watu takriban laki mbili waliuwawa na wengine zaidi ya milioni 2.5 wakalazimika kuyakimbia makazi yao tangu mzozo wa Darfur ulipozuka miaka minne iliyopita.