1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA:Viongozi wa Umoja wa Afrika wajadili kufikia suala la mageuzi katika baraza la umoja wa Mataifa

4 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEnr

Rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo amewataka viongozi wa Afrika kufikia makubaliano juu ya suala la mageuzi katika baraza la Umoja wa Mataifa.

Katika mkutano wa siku moja wa dharura wa jumuiya ya Afrika juu ya suala la Afrika kupata viti viwili vya kudumu ndani ya baraza hilo Obasanjo amesema watahitaji kushirikiana na makundi mengine.

Obasanjo pia ameongeza kusema kwaba bara la Afrika litapata hasara kubwa kuliko eneo jingine lolote lile iwapo viongozi wake hawaafikiano juu ya suala hilo.

Obasanjo anaunga mkono wazo la kufanyika mabadiliko ndani ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ili Afrika ipate viti viwili vya kudumu vyenye uwezo wa kura ya Veto ndani ya baraza hilo.

Jumuiya Afrika imegawika juu ya iwapo kukubaliano na wazo hilo au kulikiuka kuambatana na pendekezo lililotolewa na mataifa manne Brazil,India,Japan na Ujerumani la kutaka kuwepo mabadiliko kidogo katika baraza hilo lenye wanachama 15.