1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AFCON: Cameroon, Misri kuumana katika fainali

Sekione Kitojo
5 Februari 2017

Vigogo vya soka barani Afrika vivyoangukia katika hali ngumu, Misri na Cameroon vinaelekea kushuhudia hatua yao ya kufufuka vitakapokutana katika fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika Jumapili (05.02.2017).

https://p.dw.com/p/2Wzu3
Africa Cup of Nations Training Team Ägypten
Kikosi cha timu ya taifa ya MisriPicha: picture-alliance/dpa/N. Bothma

Mshindi  wa  kwanza  wa  taji  hilo  miaka  60  iliyopita Misri imekuwa  mabingwa  wa  Afrika  kwa  mara  saba  lakini  walikuwa wanarejea  tena  katika  medani  hiyo  baada  ya  kukosa  kushiriki katika  fainali  tatu  za  kombe  la  mataifa  ya  Afrika kutokana  na machafuko  ya  kisiasa   nchini  humo.

Nyuma  yao  Cameroon , pamoja  na  Ghana , mataifa  mengine yenye  mafanikio  makubwa   katika  historia   ya  mashindano  hayo yana  mataji  manne  kila  moja , ambapo  mara  ya  mwisho Cameroon  kutoroka  na  taji  hilo  ilikuwa  mwaka  2002.

African Cup of Nations Kamerun gegen Ghana
Mashabiki wa Cameroon katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika , AfconPicha: Reuters/A.-A. Dalsh

Wakati  Misri  ikionekana  kama  timu inayofanya  maajabu  baada ya  kurejea  kwake  katika  fainali  hizo  za  kombe  la  mataifa  ya Afrika  kwa  mara  ya  kwanza  tangu  kulinyakua  mara  tatu mfululizo  katika  mwaka  2006, 2008  na  2010, Cameroon ilionekana  kama  timu  ambayo  haikuwa  na  nafasi.

Wachezaji waitupa mkono Cameroon

Kutokana  na  kuathirika  na  kukataa  kwa  wachezaji  kadhaa muhimu  kukubali  kujiunga  na  kikosi  hicho  cha  Simba  wanyika cha  kocha  raia  wa  Ubelgiji Hugo Broos, badala  yake timu  hiyo ambayo  inawakosa  wachezaji  nyota  iliwaondoa  mashindanoni wenyeji  wa  michuano  hiyo  Gabon  na  vikosi vilivyoonekana kusheheni  nyota wa  kandanda   vya  Senegal  na  Ghana na kuvuka  hadi  hapa ilipofikia.

Afrika cup 2017 Gabun vs. Kamerun
Mlinzi wa Cameroon Adolphe Teikeu (kushoto) akishangiria bao pamoja na mshambuliaji Benjamin Moukandjo (kulia)Picha: Getty Images/AFP/G. Bouys

Mchezo  wa  leo  Jumapili (05.02.2017)  katika  uwanja  wenye uwezo  wa  kuingiza  mashabiki 40,000  wa Stade de L'Amitie  katika mji  mkuu  wa  gabon Libreville  utakaoanza  saa  mbili  ya  usiku kwa  saa  za  Afrika  mashariki  utatanguliwa  na  sherehe  za ufungaji  mashindano  hayo, ambazo  zitaanza saa  moja   na  nusu kabla.

Itakuwa  ni  mara  ya  tatu  kwa  timu  hizo  kukutana  katika  fainali  -- Misri  imeshinda  kwa  mikwaju  ya  penalti  mjini  Cairo mwaka 1986 na  kushinda  tena  kwa  bao 1-0  mjini  Accra  mwaka  2008.

Hiyo  ilikuwa  fainali  ya  mwisho  ya  cameroon , lakini  wakati wakiwa  na  wachezaji  kama  samuel Eto'o na  Rigobert  Song, timu yao  ya  sasa  haina  majina  makubwa   ya  nyota  wa  kandanda.

Ägypten Fußballspieler Mohamed Abou TraikaÄgypten Fußballspieler Mohamed Abou Traika
Mchezaji Mohammed Abou Trika wa Misri akishangiria bao katika fainali dhidi ya Cameroon Februari 10 , 2008.Picha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

"Kwa  wachezaji  hawa  vijana -- 14  kati  ya  23  wanacheza  kwa mara  ya  kwanza  fainali  za  kombe  la  mataifa  ya  Afrika --- inawezekana  kuwa  ni  fursa  yao adimu  katika  maisha  yao  ya kucheza  soka  kushinda  taji  hilo," Broos  alisema.

Akizungumza  na  waandishi  habari  siku  ya  Jumamosi, nahodha Benjamin  Muokandjo aliongeza: "Ni dhahiri  kwamba  wakati  ukiifika katika  kiwango  hiki  unataka  kushinda  lakini  nafikiri  ukiangalia njia  tuliyopitia  tayari  tumefanya  vizuri.

"Sifikiri  mtu yeyote  hapa  angeweza  kuagulia  kwa  kucheza  kamari senti  yake  ya  mwisho  kwetu  kabla  ya  hapa  na  hii ni aibu kubwa  kwao."

Misri  imekuwa  imara  lakini  bila  ya  kucheza  kwa ustadi  wa  hali ya  juu  katika  mbio  sake  kwenda  katika  fainali, goli  pekee walilofungwa  limekuja  katika  awamu  ya  nusu  fainali  dhidi  ya burkina  Faso.

Mlinda  mlango mkongwe

Baada  ya  kutoka  sare  katika  mchezo  huo kwa  bao 1-1,Misri walishinda  kwa  mikwaju  ya  penalti , mlinda  mlango  mwenye  umri wa  miaka  44  Essam El-Hadary  akiokoa  mikwaju  miwili  na kuwachukua  Mafarao  hao  kwenda  katika  fainali  na  kuweka matumaini  yake  hai  ya  kulinyakua  kombe  hilo  kwa  mara  ya tano   katika  kipindi  chake  akiwa  mchezaji.

Kamerun Fußball Nationalmannschaft | Torwart Fabrice Ondoa
Mlinda mlango wa Cameroon Fabrice Ondoa akishangiria ushindiPicha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Kama  Broos  akiwa  na  Cameroon , Hector Cuper  amefanya  kazi nzuri  sana  katika  kufufua  matumaini  ya  wamisri, ambao  kikosi chao  kina  wachezaji  wanne  tu  walioshiriki  katika  ushindi  wao wa  fainali  za  mwaka 2010   wakiwa  ni  El-Hadary , Ahmed Fathy, Mohammed Abdel-Shafi  na  wingi  wa  klabu  ya  Hull City Ahmed Elmohamady.

"Misri  haitakuwa  tofauti  na  vile  tulivyoiona hadi  sasa, iwapo watu  wanapenda  hivyo  ama  la, iwapo  hiyo  ina  maana tutashambulia  ama  la," Cuper alisema  siku  ya  Jumamosi.

Wakati  wake   akiwa  mchezaji Cuper  alishuhudia  nyakati za kukatisha  tamaa  nyingi  katika  fainali, mojawapo  katika  misimu mfululizo  katika   kombe  la  mabingwa  wa  Ulaya  Champions League  akiwa  na  valencia  mwaka  2000  na  2001.

Gabun Afrika Cup 2017 Senegal vs. Kamerun
Pambano kati ya Senegal dhidi ya Cameroon ambapo Cameroon ilishinda kwa mabao 2-0Picha: Getty Images/AFP/K. Desouki

Raia  huyo  wa  Argentina  ahkulienda  swali  jana  Jumamosi  juu  ya idadi  ya  fainali  alizoshiriki  na  kushindwa,  lakini  anaweza  kupata faraja  kutokana  na  rekodi  ya  Misri  katika  fainali -- wameshinda mataji  mara  saba  kati  ya  mara  nane  walizofikia  katika  fainali za  kombe  la  mataifa  ya  Afrika.

Majeruhi  wamekuwa  wakiongezeka   katika  kikosi  hicho,  hata hivyo,  na  kuna  shaka  kuhusiana  na  kushiriki  mlinzi  wa  kati Ahmed Hegazy. Washambuliaji  Ahmed Hassan  na  Marwan Mohsen wako  nje  na  Mohammed Elneny  kutoka  Arsenal  ana  maumivu  ya paja.

Fussball WM-Qualifikation Ägypten gegen Ghana
Mlinda mlango mkongwe wa Misri Essam El-hadary akiwa na umri wa miaka 44 alilinda lango la Misri vizuriPicha: Getty Images/AFP/M. El-Shahed

"Tutasubiri  hadi  dakika   za  mwisho  kuona  vipi  wachzaji  wana jisikia . Wamechoka  sana , lakini  fainali  ni  tofauti  na  michezo mingine  na  kuna  idadi  kubwa ya  mambo  katika  mchezo," ameongeza  Cuper.

Siku  ya  Jumamosi (04.02.2017) Burkina  Faso  ilijihakikishia  tuzo ya  kujifariji  ya  nafasi  ya  tatu  baada  ya  kuizaba  Ghana  kwa bao 1-0  mjini  Port-Gentil  kwa  goli  la  Alain Traore  la  mkwaju  wa adhabu  ya  mbali.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe

Mhariri: Sudi Mnette