1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Afghanistan: Tetemeko lingine la ardhi, mmoja afariki

12 Oktoba 2023

Afghanistan imekabiliwa na tetemeko jengine la ardhi leo lililosababisha kifo cha mtu mmoja na pia kusababisha hofu miongoni mwa raia

https://p.dw.com/p/4XOTg
Mkaazi wa eneo la Herat Afghanistan akifukua kifusi baada ya tetemeko mwishoni mwa juma
Mkaazi wa eneo la Herat Afghanistan akifukua kifusi baada ya tetemeko mwishoni mwa jumaPicha: Kyodo/picture alliance

Afghanistan imekabiliwa na tetemeko jengine la ardhi leo lililosababisha kifo cha mtu mmoja na pia kusababisha hofu miongoni mwa raiaambao tayari wameingiwa na kiwewe kufuatia msururu wa matetemeko yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 2 mwishoni mwa wiki.

Watu wapatao 120 wamejeruhiwa kwenye tetemeko hilo ambalo limetokea karibu kilomita 30 kaskazini mwa mji mkuu wa mkoa wa Herat, ambapo maelfu ya watu wanalala nje kwa usiku wa nne baada ya makaazi yao kusambaratishwa na matetemeko ya Jumamosi iliyopita.

Soma pia:Tetemeko la Ardhi laua watu zaidi ya 2000 Afghanistan

Afghanistan mara kwa mara hukabiliwa na matetemeko ya ardhi lakini tetemeko la Jumamosi lilikuwa baya zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha miaka 25.