Matukio na masuala ya barani Afrika yaliyozingatiwa na magazeti ya Ujerumani mnamo wiki hii ni pamoja na Mahakama ya Katiba nchini Zambia imemkataza aliyekuwa rais wa nchi hiyo Edgar Lungu, kushiriki katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2026 na hivyo kumweka kando kisiasa. Magazeti yamezungumzia juu ya ugonjwa ambao hadi hivi karibuni ulikuwa bado haujajulikana nchini Kongo. Mtayarishaji Zainab Aziz