1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini, Marekani zatoa wito wa amani nchini Zimbabwe

29 Agosti 2023

Afrika Kusini na Marekani zimetilia maanani ripoti za waangalizi wa uchaguzi nchini Zimbabwe baada ya upinzani nchini humo kudai kwamba uchaguzi huo wa rais na wabunge uliofanyika wiki iliyopita ulikumbwa na udanganyifu.

https://p.dw.com/p/4VhIN
Tume ya uchaguzi ilimtangaza Mnangagwa mwenye umri wa miaka 80 kama mshindi wa uchaguzi huo.
Tume ya uchaguzi ilimtangaza Mnangagwa mwenye umri wa miaka 80 kama mshindi wa uchaguzi huo.Picha: Jekesai Njikizana/AFP via Getty Images

Afrika Kusini na Marekani zimetoa wito wa kuzingatiwa amani nchini Zimbabwe.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC wamezitaka pande zote nchini Zimbabwe kushirikiana.

Kauli ya Ramaphosa imeonyesha kuwa serikali yake iko tayari kusaidia kuutatua mvutano kati ya serikali ya Zimbabwe inaoyongozwa na Rais Emmarson Mnangagwa na upinzani unaoongozwa na Nelson Chamisa.

Tume ya uchaguzi ilimtangaza Mnangagwa mwenye umri wa miaka 80 kama mshindi wa uchaguzi huo.

Lakini wachambuzi wametilia shaka uhalali wa matokeo hayo.