Uchumi
Afrika Kusini yaiomba China urari sawa wa kibiashara
2 Septemba 2024Matangazo
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa pamoja na Rais wa China Xi Jinping wamekubaliana kuuboresha uhusiano wao na kuwa "ushirikiano wa kimkakati wa enzi mpya", katika ziara ya Ramaphosa nchini humo.
Xi amemwambia Ramaphosa baada ya shafla ya kumkaribisha kwamba, China itahamasisha uhusiano utakaonufaisha pande zote katika maeneo ya uchumi wa kidijitali, Akili Bandia na nishati mpya.
Soma pia: Mkutano wa kilele wa China na Afrika waanza
Ramaphosa kwa upande wake amesema Afrika Kusini iko tayari kuendelea kuwa rafiki wa kuaminika wa China.
Hata hivyo, awali alimueleza Xi kwamba alinuia kupunguza nakisi ya kibiashara na Beijing, baada ya kushindwa kutekeleza ahadi ilizotoa kwenye mkutano uliopita ya kununua bidhaa za dola bilioni 300 za Afrika.