1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini yazuia matumizi ya chanjo ya Urusi Sputnik V

20 Oktoba 2021

Mamlaka ya udhibiti wa dawa nchini Afrika Kusini SAHPRA imezuia matumizi ya chanjo ya Kirusi aina ya Sputnik V, kwa uwepo wa mashaka ya kiusalama.

https://p.dw.com/p/41trE
Russland Novosibirsk | Corona-Impfstoff | Sputnik V
Picha: Kirill Kukhmar/TASS/dpa/picture alliance

Katika taarifa yake mamlaka hiyo imesema aina hiyo ya chanjo haitaruhusiwa kutumika kwa wakati huu nchini humo kwa kutolea mfano wa kushindwa kutumika kwa chanjo ya HIV, ambayo pia inatumia teknolojia inayofanana na Sputnik V.

Hata hivyo wazalishaji wa chanjo hiyo hawakuweza kupatikana mara moja kujibu hoja hiyo.

Katika utafiti uliochapishwa jarida la kisayansi la Lancet mwaka uliopita, ulionesha washiriki 20,000 walotumia chanjo hiyo walikuwa salama na kiasi ya asilimia 91 ilionesha ina uwezo wa kuwazuia watu kufikia katika hali ya umaututi kutokana na  ugonjwa wa Covid-19.