AKK akabiliwa na mbinyo katika mkutano mkuu wa chama cha CDU
22 Novemba 2019Uchunguzi wa maoni ya wapiga kura unaonesha hali mbaya kwake. Katika mkutano mkuu wa chama mjini Leipzig kwa hiyo anapaswa kuonesha hali tofauti ili kuwavutia wajumbe.
Alikuwa na mpango mkubwa , wa kukiokoa chama hicho cha CDU kutoka katika mivutano ya ndani, kukijenga upya na kujihakikishia nafasi ya mbele katika mbio za kuelekea kuwa kansela. Annehret Kram - Karrenbauer, ambaye pia anafahamika kama AKK, anabeba mfumo wake binafsi. Ametembelea matawi mashinani katika chama hicho, akizunguka nchi nzima, akijaribu kujiondoa kutoka katika taswira ya Angela Merkel, ambayo asingependa kuanza akiwa kama sehemu ya utawala wake. Badala yake anataka kujitengenezea tawira yake akiwa kiongozi wa chama cha CDU.
Lakini muda mfupi tu baadaye kila kitu kikawa wazi , mpango wake haukuweza kusonga mbele. Kama mkuu wa chama alikuwa anaonekana bila shaka mgombea wa moja kwa moja wa wadhifa wa kansela kupitia chama hicho, lakini maoni ya wapiga kura kwa upande wake yalipungua hadi nusu. Katika wanasiasa muhimu kumi wa Ujerumani, AKK ameshika nafasi ya mwisho. Kwa hiyo shaka imekuwa kubwa , iwapo inawezekana akateuliwa kuwa mgombea wa wadhifa wa kansela.
Alijikwaa mapema katika wadhifa wa mwenyekiti wa chama kwa kutoa kichekesho ambacho hakikupendeza kuhusu watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na kuharibu njia yake ya kuingia katika masuala ya dunia. Hadi wakati huo, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 57 alikuwa katika hali nzuri tu katika chama hicho ambacho viongozi wake wengi ni wanaume. AKK alijiunga na chama cha CDU mwaka 1981 akiwa mwanafunzi bado.
Ahamia Berlin
Baada ya kuingia rasmi katika masuala ya kisiasa miaka chini ya 20 iliyopita katika siasa za majimboni, alihamia mwezi Februari mwaka jana katika patashika ya siasa za taifa mjini Berlin akiwa kama katibu mkuu wa chama cha CDU. Hii ilikuwa baada ya kukiongoza chama katika mafanikio mara mbili ya ushindi wa uchaguzi katika jimbo anakotoka la Saarland.
Akiwa waziri wa mambo ya ndani na waziri mkuu wa jimbo hilo alifanya kazi nzuri sana, hadi Angela Merkel akaamua kumfuta kuja katika mji mkuu. Kazi nzuri aliyoionesha AKK katika jimbo lake alipaswa pia kuionesha mjini Berlin. Mtaalamu wa masuala ya kisiasa mjini Bonn Frank Decker anatoa tathmini yake kuhusu wadhifa wa kansela.
"Ameshindwa kuonesha kazi nzuri kama mwenyekiti wa chama, ambapo chama kinapaswa kumuunga mkono na kuwanyamazisha wakosoaji wake. Anayetaka kuingia katika mbio za kukiongoza chama , ni lazima aoneshe uwezo wake, ili aweze kuchukua pia wadhifa wa kansela."
Alianza kama mtu wa mbele kwa Angela Merkel, lakini Kramp-Karrenbauer amekuwa haraka akifanya makosa mengi. Licha ya kuwa anafahamika kuwa mzungumzaji mzuri, kuwa kiongozi wa chama amekuwa hoi mno kwa upande wa uchaguzi.Akiwa kama mkuu wa chama bila ya wadhifa wa waziri Kramp-Karrenbauer hana uzito ndani ama nje ya nchi.
Iwapo hali ya maoni ya wapiga kura itaendelea kubakia mbaya kama ilivyo, katika chama cha CDU, kuna hatari ya kutokea mivutano ndani ya chama. Ndio sababu ni lazima suala hilo lipatiwe ufumbuzi, katika miezi michache ijayo. Friedrich Merz mmoja wa watu wanaowania nafasi ya ukansela baada ya kuelezea kuwa serikali imeoza , amerejea nyuma kidogo na kueleza kuwa asingependa kufanya uasi katika serikali.
LINK: http://www.dw.com/a-51346677