1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Al-Shabaab wawauwa zaidi ya askari 50 Somalia

28 Machi 2024

Kundi la wanamgambo la Al-Shabaab linaripotiwa kuwauwa karibu wanajeshi 53 katika mashambulizi mawili katikati mwa Somalia. Wanamgambo wa kundi hilo walilipua magari yaliyojaa vilipuzi mbele ya kambi ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4eDR4
Usalama katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu
Vikosi vya usalama Somalia vinakabiliwa na wakati mgumu kupambana na wanamgambo wa Al-ShabaabPicha: Abukar Muhudin/AA/picture alliance

Kundi la wanamgambo la Al-Shabaab linaripotiwa kuwauwa karibu wanajeshi 53 katika mashambulizi mawili katikati mwa Somalia. Wanamgambo wa kundi hilo walilipua magari yaliyojaa vilipuzi mbele ya kambi ya kijeshi hapo juzi Jumanne na baada ya hapo kukashuhudiwa mapigano makali.

Soma pia: Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya 'mtandao wa al-Shabaab'

Msemaji wa serikali ya Somalia lakini anasema wanamgambo 10 waliuwawa katika shambulizi hilo. Msemaji huyo anasema wanajeshi watano pekee ndio waliouwawa. Shambulizi jengine la Al-Shabaab lilifanyika siku hiyo hiyo katika mji wa Haradhere, ambao hivi majuzi tu uliokombolewa kutoka kwa udhibiti wa kundi hilo.

Msemaji kutoka wizara ya mawasiliano ya Somalia alizungumza jana akidai kumekuwa na dazeni kadhaa ya watu waliokufa pande zote. Mashambulizi ya Al-Shabaab katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika katika miaka ya hivi karibuni yamezidi hasa katika mwezi wa mfungo wa Waislamu wa Ramadhan.