SiasaAsia
Aliyev wa Azerbaijan ashinda tena kwa zaidi ya 90%
8 Februari 2024Matangazo
Hayo ni kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta na gesi.
Aliyev amekuwa rais wa Azerbaijan tangu mwaka wa 2003, wakati alipochukuwa usukani kutoka kwa baba yake, Heydar.
Makundi ya mrengo wa kulia nchini humo yanasema uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki, madai ambayo maafisa wanayapinga.
Uchaguzi huo ulifanyika wakati kukiwa na upinzani wa ndani ya nchi, huku waandishi wa habari wakitiwa mbaroni tangu mwishoni mwa Novemba mwaka jana katika kile makundi ya haki yalisema ni ukandamizaji dhidi ya wanaoripoti kuhusu ufisadi.
Azerbaijan haikupaswa kufanya uchaguzi hadi 2025, lakini Aliyev aliuitisha mapema baada ya Baku kuchukua tena udhibiti mwezi Septemba wa mkoa wa Nagorno-Karabakh unaogombaniwa na Armenia