1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Alpha Conde wa Guinea kuwania muhula mwingine madarakani

Sekione Kitojo
3 Septemba 2020

Rais wa  Guinea Alpha Conde ametangaza kuwa anawania  muhula wa  tatu  katika  uchaguzi  wa   hapo Oktoba 18, akithibitisha  mipango  ambayo  ilitarajiwa  kwa muda  mrefu

https://p.dw.com/p/3hwOk
Guinea Präsident Alpha Condé
Picha: Getty Images/C. Binani

Rais wa  Guinea Alpha Conde ametangaza kuwa anawania  muhula wa  tatu  katika  uchaguzi  wa   hapo Oktoba 18, akithibitisha  mipango  ambayo  ilitarajiwa  kwa muda  mrefu  ambayo  imezusha  machafuko yaliyosababisha  watu  kuuwawa.

Sasa nina  nia, kwasababu  nyie ndio mlioamua  kuwa napaswa  kuonesha  nia, kiongozi  huyo  mwenye umri  wa miaka  82 alisema  katika  mkutano  kwa  njia  ya  vidio kwa waungaji  mkono  wanawake  wanaofanya  kampeni  kwa ajili  yake  ili  kugombea  tena.

Conde, akiwa  mwishoni mwa  muhula  wake  wa  pili  na wa  mwisho  madarakani,  alisukuma  mabadiliko  ya  katiba mwaka  huu  ambayo  wapinzani  wanasema  yalipangwa kubadilisha  muda wa  kugombea.

Maandamano  dhidi  ya  mpango  wake  ulioshukiwa wa kugombea  tena  yalizuka  katika  taifa  hilo  la  Afrika magharibi Oktoba mwaka  jana  lakini  yalikumbana  na ukandamizaji wa  nguvu, na  watu  kadhaa  walipoteza maisha.