1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty yaihimiza Kongo kusitisha hukumu ya kifo

9 Januari 2025

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limetoa mwito kwa Rais Felix Tshisekedi kusitisha utekelezaji wa hukumu ya kifo kwa watu kadhaa waliopatikana na hatia.

https://p.dw.com/p/4oyUP
 Amnesty yatoa mwito kwa Rais Tshisekedi kusitisha utekelezaji wa hukumu ya kifo kwa watu kadhaa waliopatikana na hatia.
Amnesty yatoa mwito kwa Rais Tshisekedi kusitisha utekelezaji wa hukumu ya kifo kwa watu kadhaa waliopatikana na hatia.Picha: Pond5 Images/IMAGO

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limetoa mwito kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Felix Tshisekedi kusitisha utekelezaji wa hukumu ya kifo kwa watu kadhaa waliopatikana na hatia ya kushiriki kwenye magenge ya wahalifu.

Shirika hilo limenukuu ripoti zinazoeleza kwamba zaidi ya watu 170 wamepangwa kunyongwa nchini humo.

Mkurugenzi wa Amnesty International kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Sarah Jackson amezitaja taarifa hizo za watu kunyongwa kuwa za ''kushtua.''

Mamlaka nchini Kongo zimewahukumu mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa magenge ya wahalifu, wanaojulikana kama kulunas, kama sehemu ya oparesheni kubwa dhidi ya magenge ya wahalifu.

Wengi wao wanakabiliwa na hukumu ya kifo kwa makosa ya kufanya uhalifu kwenye maeneo ya mijini na wanashikiliwa katika magereza yenye ulinzi mkali.