ANC yaadhimisha miaka 112 ya kuasisiwa kwake Afrika Kusini
13 Januari 2024Chama tawala nchini Afrika Kusini African National Congress - ANC kinasherehekea leo miaka 112 ya kuasisiwa kwake kabla ya kufanya uchaguzi wa kitaifa, unaotarajiwa kuwa mkali zaidi tangu kilipoingia madarakani katika mwaka wa 1994.
Soma pia: Ramaphosa mwenyekiti tena chama tawala ANC
Maelfu ya wanachama na wafuasi wanatarajiwa kukusanyika katika Uwanja wa Michezo wa Mbombela katika mkoa wa Mpumalanga ambako Rais Cyril Ramaphosa, ambaye pia ni mkuu wa chama wa ANC, atatoa hotuba yake ya mwaka na kutangaza mpango wa chama hicho kwa mwaka huu.
Soma pia: Chama cha ANC chagawanyika katika makundi yanayomuunga mkono na yanayompinga Ramaphosa
Ramaphosa anatafuta muhula wa pili katika uchaguzi wa mwaka huu baada ya kuingia madarakani katika mwaka wa 2019, akichukua usukani kutoka kwa Jacob Zuma. ANC imekuwa ikikabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa kushindwa kutoa huduma za msingi kwa mamilioni ya raia weusi maskini walio wengi, wakati kukiwa na mazingira yanayozorota ya kiuchumi.