ANC yaelekea kupoteza wingi wa kura Afrika Kusini
30 Mei 2024Matokeo hayo yanayoongeza uwezekano kwa chama hicho kupoteza kwa mara ya kwanza wingi wa viti bungeni tangu kiliposhika hatamu za dola miaka 30 iliyopita.
Hadi sasa katika asilimia 20 ya kura zilizokwishahesabiwa, ANC kimepata asilimia 43 kikifuatiwa na chama cha Democratic Alliance kinachokaribia asilimia 30.
Soma pia:Afrika Kusini yasubiri matokeo ya uchaguzi mkuu
Chama cha mwanasiasa machachari Julius Malema na kile cha rais wa zamani Jacob Zuma cha uMkhonto weSizwe vimeambulia chini ya asimilia 10 ya kura.
Iwapo ANC itashindwa kupata asilimia 50 ya kura italazimika kutafuta mshirika kutoka vyama vingine vidogo ili kuunda serikali. Matokeo hayo yatadhihirisha kuanguka kwa umashuhuri wa chama hicho tangu kulipoingia madarakani mwaka 1994 chini ya hayati Nelson Mandela.