ANC yashindwa kupata wingi wa kura bungeni
1 Juni 2024Kushindwa huku kumetokea kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 30 ya utawala wa demokrasia nchini humo.
Takriban asilimia 99 ya kura tayari zimeshahesabiwa na chama hicho kinachoongozwa na rais Cyril Ramaphosa kimepata asilimia 40 ya kura kikiwa kimepoteza sana ukilinganisha na uchaguzi uliopita wa mwaka 2019 kilipopata asilimia 57.5 ya kura.
Huenda Afrika Kusini ikaunda serikali ya mseto
Kwa sasa chama hicho kitahitajika aidha kuwa na serikali ya mseto, au kuvishawishi vyama vingine kumuunga mkono Ramaphosa kuchaguliwa tena bungeni ili kumruhusu kuunda serikali ya wachache ikishirkiana na vyama vingine kupitisha bejeti na sheria nyengine bungeni.
Katibu Mkuu wa ANC Nomvula Mokonyane amesema halmashauri kuu ya chama hicho itakutana kuamua hatua za kuchukua baada ya matokeo rasmi kutangazwa.