1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ankara:al-Qaida wahusishwa na mashambulio ya Istanbul:

18 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CG04

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uturuki, Abdullah Gül, amesema tuhuma zinazidi kupata nguvu kuwa mtandao wa kigaidi wa al-Qaida unahusika na mashambulio mawili ya kujitolea mhanga ya masinagogi mawili mjini Istanbul. Amesema mjini Ankara kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuhusu tuhuma hizo. Gazeti la lugha ya Kiarabu, linalochapishwa mjini London, limepokea barua pepe juzi Jumapili iliyosema kuwa mtandao wa al-Qaida unahusika na mashambulio hayo. Idadi ya watu waliofariki kutokana na mashambulio hayo ya Jumamosi iliyopita imeongezeka na kufikia 25. Watu wengine 300 wamejeruhiwa. Polisi wa Uturuki wamewatambua wauaji wawili wa kujitolea mhanga nao ni Waislamu wa Kituruki wenye itikadi kali. Maiti zao zinafanyiwa uchunguzi kabla ya kuzikwa.