Annan asikitishwa na mapigano mapya Mashariki ya Kati
25 Septemba 2005Matangazo
New York:
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, amekosoa vikali kupamba moto kwa machafuko mapya katika Mashariki ya Kati. Amesema mjini New York kuwa ana wasiwasi mkubwa na kile kinachotokea kwani uwezekano wa kuafikiana baada ya Waisraeli kuondoka katika Ukanda wa Gaza huenda ukasambaratishwa. Wakati huo huo, amewaomba Wapalestina kutekeleza kikamilifu mwito wa Rais wao, Mahmoud Abbas wa kujenga jamii ya kidemokrasia. Wanajeshi wa angani wa Israeli wameyashambulia malengo ya Wapalestina jana na usiku wa kuamkia leo baada ya Wapalestina wenye itikadi kali kushambulia mji wa mpakani wa Zderot. Mashahidi wamesema kuwa Wapalestina kadhaa wameuawa na kujeruhiwa.