Annan ataka kipelekwe kikosi cha amani Burundi
20 Machi 2004Matangazo
NEW YORK: Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan ameliita Baraza la Usalama lipeleke kikosi cha kuhifadhi amani nchnini Burundi. Nchi hiyo ya Afrika ya Kati ina nafasi nzuri wakati huu kurejeshewa hali yake ya usalama miaka kmumi baada ya kumalizika vita vya ndani. Kwa ajili hiyo hadi hapo tarehe 2 April UM utapaswa kupokea dhamana ya hifadhi ya amani kutoka nchi za UA. Bwana Annan ameshauri kipelekwe kikosi cha wanajeshi 5,650 cha UM. Baraza la Usalama la UM litaijadili hali ya Burundi hapo Jumatatu.