1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annan atoa mwito wa kusaidiwa Iraq:

14 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFsS

Hamburg: Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan ameiita jamii ya kimataifa ianzishe juhudi ya pamoja za kuisaidia Iraq. Siyo tu hali ya mtafaruku nchini Iraq itahatarisha amani katika eneo hilo zima bali huenda ikaitumbukiza dunia nzima katika mgogoro, Bwana Annan aliliambia jarida la Kijerumani DER SPIEGEL. Katibu Mkuu huyo wa UM alisema swali la kurejea watumishi wa UM nchini Iraq litaendelea kutegemea juu ya kuhakikishwa hali ya usalama nchini humo. Wakati huo huo Bwana Annan alilaumu tena ule uamuzi wa Marekani wa kuyanyima makampuni ya nchi zinazopinga vita haki ya kushiriki katika ukarabati wa Iraq. Waziri wa Mambo ya Maendeleo wa Ujerumani Bibi Heidemarie Wieczorek-Zeul alisema shauri la Marekani kwamba Ujerumani iifutie Iraq madeni yake litategemea juu ya kufutwa kwa uamuzi wake huo. Rais George W. Bush wa Marekani aliziita Ujerumani, Urusi na Ufaransa ziisaidie Iraq kwa kuifutia madeni yake.