Annan azungumza na Bush na Powell
20 Desemba 2003Matangazo
NEW YORK: Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan amezungumza na Rais wa Marekani George W. Bush na Waziri wa Mambo ya Nje Colin Powell juu ya maandalizi ya kukutana na Baraza la Utawala la Iraq. Habari za wanadiplomasia zilisema viongozi hao wawili wamesema wanakaribisha mkutano huo utakaofanyika Januari 15 katika makao makuu ya UM mjini New York. Hata hivyo bado hawakuahidi kushiriki katika mkutano huo. Katibu Mkuu wa UM angependelea mazungumzo ya mkutano huo yatuwame juu mchango wa UM kuhusu swali la ukarabati wa Iraq. Bwana Annan amemwalika kuhudhuria mkutano huo Adnan Patshatshi atakayeshika wadhifa wa Rais wa hilop la Utawala kuanzia Januari mwakani. Akikaribisha mwaliko wake Bwana Patshatshi alisisitiza kuwa mashauriano ya UM yangechangia sana katika utungaji wa mswada wa katiba pamoja na maandalizi ya uchaguzi mkuu nchini Iraq.