Antonio Gutteres: vita dhidi ya wanamgambo vinatatizwa Sahel
26 Septemba 2019Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres amesema kuwa Afrika Magharibi na nchi zenye nguvu katika Jumuiya ya Kimataifa zinashindwa katika juhudi za kukabiliana n akitisho cha kundi la wanamgambo wanaojiita dola la kiislamu katika eneo la Sahel ambalo linasambaa kuelekea ghuba ya Guinea .
Makundi yanayoshirikiana na al-qaeda na kundi hilo linalojiita dola la kiislamu, yameimarisha juhudi zao katika eneo kame la Sahel mwaka huu na kufanya maeneo mengi ya ngome zao kutoweza kusimamiwa na uongozi na kusababisha ghasia hasa nchini Mali na Burkina Faso.
Ufaransa iliyokuwa nguvu ya kikoloni katika eneo hilo , iliingilia kati hali nchini Mali mwaka 2013 kuwafurusha wanamgambo wa kundi linalojiita dola la kiislamu lililokuwa limeteka eneo la Kaskazini, lakini badala ya kuliimarisha eneo hilo, hali imezidi kuwa mbaya.
Viongozi wa Afrika Magharibi wameahidi kutoa dola bilioni 1 kukabiliana na kitisho hicho lakini kutokana na madai kuhusu ufadhili wa awali, hatua hiyo inatiliwa shaka.